Gari moja aina ya Coaster ambalo lilikuwa likielekea kwenye Show ya Nandy Festival mkoani Sumbawanga limepata ajali Mikumi mkoani Morogoro usiku wa jana na baadhi ya watu ambao hawakutambulika mara moja wamekimbizwa hospitali kwaajili ya matibabu.
Msafara huo una wasanii kadhaa wakiwemo Juma nature, Whozu, Stamina, Nandy , Barnaba , Roma , Billnass , Ice Boy na msanii kutoka Kenya Willy Paul. Taarifa kamili itakuja.