Mwanadada aliyetia fora UCL final kati ya Tottenham na Liverpool

Mwanadada Kinsey Wolanski, ambaye alivamia uwanjani wakati wa mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu mbili kutoka England Tottenham na Liverpool usiku wa kuamkia leo nchini Uhispania ameeleza sababu zilizomfanya afanye tukio hilo ambalo lilisimaisha mchezo kwa dakika kadhaa.

Mwanadada huyo ambaye ghafla alikatiza kwenye mabango ya matangazo katika dimba la Wanda Metropolitano na kuvamia uwanja amesema nia yake ilikuwa ni kutangaza bidhaa ya mchumba wake inayoitwa Vitaly Uncensored.

“Maisha ni kuishi, fanya vitu vikubwa ambavyo vitaacha kumbukumbu ya milele,” aliandika mwanadada huyo huku akiijumuisha na kipande cha video kinachoonesha akivamia uwanjani na kutolewa na wanausalama wa uwanjani.

Halafu baadaye akaposti picha akiwa anatolewa nje huku mchezaji wa Spurs Harry Winks akimwangalia na kuandika: “Je, nilimuharibia siku yake huyu #8 kwa kiasi Fulani?”

Baadaya tukio hilo, akaunti zake za mitandao ya kijamii zilimiminika komenti na kumfanya kupata wafuasi wapya 900k kutoka makumi ya wafuasi ndani ya muda mfupi tu.

Baada ya tukio hilo mchmba wake Vitaly Zdorovetskiy, mfanya vituko maarufu kwenye YouTube ambaye aliwahikuvamia uwanja wakati wa Fainali ya Kombe Dunia mwaka 2014, ameweka posti yenye ujumbe unaosomeka kwamba atamuo mwanadada huyo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *