Msanii wa Injili Mr. Seed amejiondoa kwa mtandao wa kijamii.
Baba wa mmoja amejiondoa kwa mtandao siku moja baada kushtumiwa kufanya mapenzi nje ya ndoa na mwanadada mmoja.
Mwanadada huyo alitoa madai kuwa Mr. Seed alimlazimisha kufanya ngono naye jambo ambalo limewashangaza wengi.
Itakumbukwa kuwa Mr. Seed alijing’atua kwenye studio ya kurekodi mziki wa EMB kwa madai ya unyanyasaji kutoka kwa bosi wake wa zamani Bahati Kenya.
Baada ya kutunga nyimbo ya Upo mwezi jana, ambapo aliangazia suala nyingi hadi ya kujitia kitanzi miongoni mwa masahibu aliyoyapitia, inaoenekana masihara bado yanamwandama.
Kashfa nyingi zimeripotiwa kutoka sekta ya injili na inauma sana kuona nchi ikienda kuzama kwa uozo wa jamii na vijana kwa jumla.
Hata hivyo, sidhani kutoa ukurasa wa Instagramu ilikuwa murwa kwa Mr. Seed badala ya kuiangalia suala yenyewe ana kwa ana.
Kutoka skendo hii, inaonekana msanii Bahati atakuwa kwa kicheko baada ya kukuwa na tofauti na Mr. Seed kwa muda na kwamba amekuwa akisema ‘vijana hao’ anawadai zaidi ya shilingi milioni sita.
Hii mkondo aeichukua ni ile ile ilichukuliwa na rais Uhuru Kenyatta baada ya Wakenya kumsuta na masuala zinazosumbua kama wananchi.
Rais Uhuru kwa sasa amejiondoa kwa mitandao zote na kwa mtandao wa Twitter alikuwa rais mwenye wafuasi wengi kote Africa.