Pwagu Kapata Pwaguzi! Mwizi Ahepa na Hongo ya Polisi

Mwizi mmoja jasiri maeneo ya Embu amegonga vichwa vya habari baada ya kuhepa na pesa za hongo kutoka kwa polisi wa trafiki.

Kulingana na shahidi aliyeongea na Daily Nation, mwizi huyo  alitoka kwenye msitu uliokaribu na kutoweka na kifungu cha pesa kwenye barabara kuu ya Meru na Nairobi.

Kwa mujibu wa shahidi huyo aliyekuwa akiendesha gari lake kwa upande mwingine wa barabara, polisi hao walikuwa wawili, wa kike na wa kiume.

Polisi alipigwa na butwaa aliposhindwa kumkimbiza mwizi huyo na akamtemea matusi.

“Kuna barabara hizi zenye mwinuko ambazo zinaunganisha barabara kuu ambapo maafisa walikuwa wamesimama wakikagua magari. Hiyo ndiyo barabara ambayo mwizi alitumia kutoroka. Afisa aligundua kuwa hangeweza kumshika yule kijana na akabaki tu akichemka na matusi, “shahidi huyo alisema.

Polisi hao hawakuwa wamejihami na bunduki na ikawapelekea kupoteza ‘windo’ lao la siku.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *