Beatrice Chepkoech Aishindia Kenya Dhahabu

Mumiliki wa rekodi ya dunia Beatrice Chepkoech amefanya kazi nzuri baada ya kunyakua medali ya dhahabu katika fainali ya mbio za kuruka viunzi na maji vya mita 3000. Ushindi huu ulishuhudiwa katika kwenye Mashindano ya riadha ya Dunia ya IAAF huko Qatar, Doha.

Chepkoech alivuka safu ya kumaliza kwa wakati wa 8:57:84, mbele ya Emma Coburn wa USA ambaye alimaliza kwa wakati 9:02:35 na Gesa Felicitas Krause wa Ujerumani ambaye alimaliza wa tatu kwa saa 9:03:30.

Hyvin Kiyeng alimaliza wa nane kwa wakati 9:13:53 huku mwenzake Celliphine Chepsol akijiondoa kwenye mbio katikati.

Chepkoech, ambaye alionekana kukata shauri ya ushindi tangu kuanza alisonga mbele ya wenzake nakuwaacha kwa mita 30

Amekuwa akisubiri kwa miaka miwili kwa nafasi yake ya kurekebisha kile kilichotokea London ambapo alielekea kwenye Mashindano ya Dunia baada ya kukosa kuruka maji ana kulazimika kuridi nyuma na kupoteza wakati katika harakati ile.

Chepkoech alijikomboa kwa kuvunja rekondi ya Dunia kwa wakati 8:44.32 nchini Monaco mwaka uliofuata.

“Ninaomba tu kuwa na afya njema tunapoelekea kwenye ubingwa wa Dunia. Ninaahidi kukimbia kama timu na kuishindia Kenya dhahabu, “alisema Chepkoech kabla ya Mshindano ya Doha.

Kwa kweli sala zake zimejibiwa. Hongera Beatrice!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *