Shoka La Magoha Lapiga Tena, Afunga Shule Nyingine

Waziri wa elimu George Magoha leo hii ameendeleza shughuli ya Kuzifunga shule zisizo salama kwa wanafunzi.

Magoha akiwa kwenye ziara yake huko Changamwe, aliamuru kufungwa kwa Chuo cha Greenfield ambacho muundo wake ulipataikana kuwa hatari kwa wanafunzi.

Shule hii iliyo katika Kaunti ya Mombasa ni shule ya nne kusitisha huduma zake kufuatia msiba uliotokoea katika Shule ya Precious Talents kule Dagoretti.

Katika kisa cha awali,  Magoha ambaye aliambatana na Katibu Mkuu wake, Belio Kipsang, aliamuru uhamisho wa wanafunzi 207 kutoka Bombolulu hadi shule jirani, Ayany Estate Primary.

“Watoto kutoka Bombululu watahamishiwa hadi shule hii (Ayang) kwa sababu ina nafasi za ziada,” alitangaza.

Magoha pia alifichua kuwa jengo hilo (shule ya Bombolulu) halikuwahi kuidhinishwa na mtu yeyote na majengo hayo pia hayakusajiliwa.

Katika hotuba yake, Magoha aliisihi jamii kuelewa kwamba wizara hiyo inafanya kazi kwa sababu ya maslahi ya watoto.

Wakati ziara ya ukaguzi wake, CS aligundua kuwa walimu katika shule ya Bombolulu hawakuwa wamesajiliwa na TSC, ikilinganishwa na Ayang ambayo ilikuwa na zaidi ya waalimu 27 waliosajiliwa.

Pia aliwapa uwezo maksusi maafisa kufunga shule yeyote amabyo ilikuwa katika hali sawia na St. Catherine Bombolulu.

“Kuanzia sasa hakuna mtu anayepaswa kuningojea mimi kufunga shule yoyote ambayo inaonekana kuwa katika hali mbaya sawia na tulioifunga. Nimewapa nguvu maafisa wangu kuzifunga shule hizo lakini kwa hali ya uadilifu,” alifafanua.

Magoha alitembelea eneo la mkasa  kutoa rambirambi kwa wakaazi na pia kuweka wazi hatua itakayochukuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *