Jose Chameleone apata kibali cha kimataifa kabla ya 2021

Image result for chameleone awarded in African descent festival

Msanii wa Afro Beat Joseph Manyanja almaarufu Jose Chameleone ambaye kwa muda usio mrefu alitangaza azma yake ya kuingia kwenye siasa kabla ya mwaka wa 2021 ametuzwa ughaibuni.

Chameleone aliyejiunga na chama mzee cha Democratic Party (DP) alituza kwa kusaidia kukuza jamii kwa kupitia usanii wake na kuimarisha umoja.

Msanii huyo alipata tuzo kwenye tamasha la African Descent Festival vancouver nchini Canada ambapo kulikuwa na mazungumzo juu ya kutumia usanii kwa kukuza jamii.

Image result for chameleone awarded in African descent festival

“Ni kwa heshima sana nimetuzwa na tuzo la kimaisha kwenye tamasha ya African descent festival kwa mchango wangu mkubwa kwenye mziki wa Afrika,” Chameleone alisema pindi tu alipopokea tuzo.

Jose Chameleone alitagaza hivi majuzi kuhusu azimio lake la kumng’atua Bwana Meya Ssalongo Erias Lukwago kwenye uchaguzi mkuu wa 2021.

Chameleone alipokelewa vizuri kwenye chama cha DP kinachoongozwa na Norbert Moa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *