Kagere, Nyoni wang’aa MO SIMBA AWARDS 2019

Leo Alhamisi usiku klabu ya Simba imetoa uzo kwa wachezaji wake waliofanya vizuri msimu  huu uliomalizika wiki hii Jumanne Mei 28, 2019, tuzo ambazo zinajulikana kwa jina maarufu la ‘Tuzo za Mo’. Tuzo hizi zimeandaliwa na mwekezaji wa klabu hiyo Mohamed Dewji na alianza utaratibu huo msimu uliopita kwaajili ya kuwapa motisha wachezaji waliofanya vizuri na hata wale ambao hawakupata nafasi ya kutosha kucheza basi kuongeza juhudi ili msimu ujao wafanye vizuri zaidi.

Tuzo hizo zimegawanywa katika vipengele 11 ambavyo ni kipa bora wa mwaka, beki bora wa mwaka, kiungo bora wa mwaka, mshambuliaji bora wa mwaka, goli bora la mwaka, mfungaji bora wa mwaka, tuzo ya wachezaji, mchezaji bora wa mwaka, tuzo ya heshima, mchezaji bora mdogo na mchezaji bora wa kike.

Katika tuzo hizo hizo Beki Bora wa Mwaka amekuwa ni Erasto Nyoni, Kiungo Bora wa Mwaka amekuwa ni James Kotei, Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka imeenda kwa John Bocco, Goli Bora la Mwaka limeenda kwa Clatous Chotta Chama, Mfungaji Bora wa Mwaka ni Meddie Kagere.

Tuzo nyingine ni Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka imeenda kwa Rashid Juma, Tuzo ya Wachezaji imeenda kwa Erasto Nyoni, Tuzo ya Heshima amechukua Azim Dewji, Mchezaji Bora wa Mwaka Meddie Kagere, Kipa Bora wa Mwaka ni Aishi Manula, Mchezaji Bora wa Kike ni Mwanahamisi Omary Shurua.

Kwa mgawanyo huo wa tuzo, Meddie Kagere ndiyo wanufaika wakubwa zaidi baada ya kila mmoja kujinyakulia tuzo mbili.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *