Mwanaume aliyempa mimba mwanafunzi wa darasa la nne bado hajafahamika

Mwanaume aliyempa ujauzito mwanafunzi wa darasa nne mwenye umri wa miaka 11 ambaye aliacha shule baada ya kubainika ana ujauzito wa miezi saba bado hajafahamika.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa anasoma katika shule ya msingi Waelezo iliyopo katika Halmashauri ya Shinyanga ilimlazimu kukatisha elimu hiyo baada ya kugundulika ana ujauzito wa miezi saba.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri, Elizabeth Mweyo, wakati wa kikao cha wenyeviti wa vitongoji 30 alieleza kuwa mwanafunzi huyo alipatiwa ujauzito mwaka jana na mwanaume ambaye hajafahamika.

Alisema mwanafunzi huyo aliendelea na masomo baada ya muda mwalimu wake alimgundua na kwenda kumpima ndipo ikagundulika na ujauzito.

Aidha, alisema lengo la kukutana kwa pamoja ni kujadili na kupanga njia bora za kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwani bado tatizo ni kubwa.

 

“Watoto hawafikii ndoto zao kama tukio la mwanafunzi wa darasa la nne ameshindwa kuendelea na elimu yake baada ya kugundulika ni mjamzito,” alisema

Naye Ofisa Mtendaji wa kata ya Usanda, Emmanel Maduhu, amewataka wenye viti wa vitongoji kutumia sheria za kimila kuwaadhibu wanaume wanaowapa mimba wanafunzi ili matukio hayo yasiendelee kutokea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *