Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Bandari

 

Leo tarehe 10 Agosti, 2023, Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imefikia uamuzi wa kufuta kesi inayopinga mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai.

Mahakama imethibitisha mkataba wa IGA kuwa halali na imeeleza kuwa malalamiko yaliyotolewa hayana msingi.

Kesi namba 5 ya mwaka 2023 iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na mawakili Alphonce Lusako, Emmanuel Chengula, Raphael Ngonde na Frank Nyalus imefikia uamuzi huo.

Jaji Dastan Ndunguru alisoma hukumu hiyo akieleza kuwa baada ya majaji watatu kusikiliza pande zote, mahakama imebaini kuwa hoja sita zilizotolewa hazina msingi, hivyo mkataba wa IGA haukuwa na kasoro za kufanya usitekelezwe.

Malalamiko yalijikita katika misingi minne:

  • Mkataba haukutolewa kwa umma wala kushirikisha wananchi kabla ya kuridhiwa.
  • Mkataba uliosainiwa ulidaiwa kukiuka sheria.
  • Mkataba ulikuwa kinyume na maslahi ya umma na rasilimali za umma.
  • Mkataba ulionekana kuwa na vifungu vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi.

Wakili wa walalamikaji, Bonifasi Mwabukusi, alizungumza na waandishi wa habari akieleza nia yao ya kukata rufaa, kwani hawakubaliani na uamuzi wa mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *