Mwasiti Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake na Kuzaa

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti mwanana, Mwasiti amefunguka kuhusu maisha yake ya mahusiano na familia kufuatia watu wengi kuhoji kuhusu maisha yake

Akizungumza na East Afrika Radio jana Februari 13 Mwasiti alisema kuwa, kwa aina ya maisha anayoipenda, anainjoi sana watu wasipojua kuhusu maisha yake binafsi.

“Wewe niambie unachotaka kujua kuhusu mziki wangu, ntachimbua mpaka chini ya uvungu,” alisema mwasiti

“Kuna wengine wananiambia kwa nini hutaki kuzaa, unajuaje kama mimi sijazaa? Au kwa sababu sijaweka instagram tumbo” aliongeza mwasiti

Mwasiti alifunguka kuwa mpenzi anaye lakini anaweza kuja kuolewa au ikawa tayari alishaolewa na watu wasijue

Mwasiti aliweka wazi kuwa, yuko kwenye mahusiano mazuri, yanampa raha, yanampa heshima, yanamfanya afanye kazi yake kwa uzuri kabisa bila malalamiko yoyote.

Amesema, mpenzi wake aliyenaye atakuwepo kwenye video yake mpya inayotarajiwa kutoka hivi karibuni ya wimbo wa ‘Raha’.

Kuhusu wimbo wa Raha anasema ameuandika mwenyewe na alitaka uwe wimbo wa tofauti ambao mtu akiusikia atafurahi na sio kuhuzunika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *