Babu Owino Anyimwa Dhamana

Image result for Babu owino

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino alishtakiwa katika Korti ya Sheria ya Milimani Jumatatu, Januari 20 baada ya kukamatwa kwa kumpiga risasi DJ Evolve huko B-Club, Nairobi Ijumaa, Januari 17.

Mbunge huyo alikataa mashtaka yaliyotolewa dhidi yake ambayo ni ya kukusudia kutekeleza mauaji, ambayo hukumu yake ni kifungo cha maisha.

Jaji Francis Andayi aliamuru kwamba Babu achikiliwe kwa siku saba zaidi kungoja kesi hiyo kutajwa mnamo Jumatatu, Januari 27.

Babu aliwakilishwa na, miongoni mwa wengine, mawakili Cliff Ombeta na Danstan Omari.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa Babu hakuwa mgeni kwenye vyumba vya mahakama, na kuonyesha tumaini la kupata haki.

Jaji alielezwa kwamba tabaka ya mbunge huyo ingemwezesha kubadilisha mkondo wa kesi na hata kutishia mashahidi wa kesi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *