Aisha Jumwa Atoa Tamko Baada ya Kiunjiri Kufutwa

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amewasihi wafuasi wake kugoma mazungumzo ya umma wa Mpango wa  BBI.

Katika video aliyochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii,  mbunge huyo aliyejaa hamaki aliwasihi wakaazi wa Malindi kutojihusisha na ripoti inayopendekezwa kufuatia kupigwa kalamu kwa aliyekuwa  Waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri.

Jumwa alieleza sababu ya wito huo ni kutokana na kikosi kilichokuwa kikiendeleza majadiliano ya BBI kutowahusisha viongozo wote akiwemo yeye.

“Ninawasihi wakaazi wa Pwani, haswa WaMijikenda, kwamba hatupaswi kuongea juu ya BBI. Tumeonyeshwa kuwa haiko juu yetu. Kwa nini tuijadili ?

“Ninakuomba kwa sababu ninahisi uchungu. Tunahitaji kuongea ili sauti zetu zisikike,” alisema Jumwa.

Kufutwa kwa Kiunjuri, ambaye ni mwandani wa karibu wa Rais William Ruto, kama Jumwa, inakadiriwa kuwa imesababishwa ufa naozidi kunoga  kati ya Uhuru – na viongozi wanashiriki na Ruto.

Tazama Video

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *