Seneta wa Kundi la Tanga Tanga Akamatwa

Image result for Samson Cherargei

Seneta wa Nandi Samson Cherargei amekamatwa baada ya kunena matamshi ya chuki mnamo mwezi Agosti.

Cherargei alikamatwa Jumanne, miezi nne baada ya kurekodi taarifa katika ofisi za DCI katika kaunti ya Kisumu.

Anatarajiwa kufikishwa kortini Jumanne kukabiliana na mashtaka ya chuki ya kikabila.

Wachunguzi walisema kwamba seneta huyo alitamka maneno ya chuki katika Shule ya Msingi ya Kilibwoni mnamo Agosti 17.

Baadaye aliachiliwa kwa dhamana ya kibinafsi.

Seneta alijitetea kwa kusema kwamba maneno aliyoyatoa kuhusu kuunga mkono Naibu Rais William Ruto, 2022, na ambayo yalisababisha kukamatwa kwake, yalinukuliwa vibaya.

Alieleza wapelelezi wa DCI Kisumu walipomuuliza kuhusu  maana ya maneno aliyotumia.

Seneta aliwataka wapelelezi wa serikali wasite kumtishia.

Cherargei alisema kwamba alikuwa akichunguzwa kwa sababu ya msimamo wake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Haki, Masuala ya Sheria na Haki za Binadamu.

Seneta alihoji nia ya wapelezi wao kwani tangu kumkamata hawajamfungulia mashtaka.

“Nashangaa kuwa watu hawa hawajanipeleka kortini. Wanataka kunitishia kwa kuandika taarifa, huku wakinitishia kunikamata kwa mashataka ya jinai,” Cherargei alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *