Mariga Aviacha Vinywa wazi Baada ya Kununua Mchoro Pesa Nyingi Kibra

Mgombea wa Chama cha Jubilee katika uchaguzi mdogo Kibra leo Jumapili, Septemba 29,  amekuwa gumzo baada kutumia pesa nyingi kwa kipande cha sanaa huko Kibra.

Akiungana na seneta mteule Millicent Omanga, mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie – ambaye alikuwa kiongozi wa sherehe hiyo- na viongozi wengine kadhaa wa chama cha Jubilee, Mariga aliingia katikati ya kitongoji hicho duni, na kuwaacha wengi kinywa wazi baada ya kulipia pesa nyingi kwa mchoro.

Kiarie (anayejulikana kama KJ), aliona kijana mdogo akiwa na mchoro wa picha ya Mariga, akiwa katikati ya halaiki ya watu waliokuwa wamefurika kumwona mchezaji huyo tajika.

Jubilee Party's McDonald Mariga speaking to the residents of Kibra on September 29, 2019

Msanii huyo mchanga aliletwa kwenye jukwa na walinzi wa usalama na KJ akamtaka auunue uchoraji huo ili kila mtu aliyekuepo kuona.

Mbunge wa Dagoretti Kusini – anayejulikana kwa kukuza wasanii baada ya kutengeneza jina lake katika uwanja wa sanaa pia- alinunua uchoraji kama zawadi kwa Mariga.

“Mimi ni msanii na hii picha nanunulia Mariga aweke kwa ofisi yake ya CDF kwa shilingi elfu kumi”

Mariga aliyeonekana kuvutiwa alisonga mbele ya jukwa na kuongeza Ksh 50,000 kwa bei hiyo, akimkumbatia msanii huyo mchanga, na umati wa watu ukishangilia.

Kufikia wakati msanii huyo akitoka kwa jukwaa, alikuwa na utajiri wa Ksh 105,000, na seneta Omanga aliongeza Ksh 20,000 na viongozi wengine kadhaa, kwa mshikamano na mgombea wa chama chao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *