Marehemu Tob Cohen hatimaye amezikwa kwenye Makaburi ya Wayahudi jijini Nairobi. Kati ya waliokuwepo katika mazishi ya mfanyabiashara huyo alikuwa ni mkewe, Sarah Wairimu, ambaye pia ni mtuhumiwa mkuu katika mauaji yake.
Akihudhuria mazishi hayo chini ya ulinzi mkali, Wairimu alitoa usemi mzito na kumuomboleza bwanake Cohen .
“Kifo cha Cohen kimekuwa kikiniumiza sana. Kifo kimeninyang’anya mtu jasiri na mpendwa.”
Alimuomba mungu kuhakikisha kuwa haki ilitendeka na wahalifu waliotekeleza mauaji hayo wamepatikana. Pia, alisema kuwa amewasamehe wale ambao wameamua kumhukumu vibaya.
Mwili wa Cohen ulihamishwa kutoka kwa eneo la kuhifadhia maiti la Chiromo hadi kaburi la Wayahudi kwenye barabara ya Wangari Maathai kwa ibada za mwisho. Baadhi ya watu maarufu waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na balozi wa Uholanzi na binamu za Rais Uhuru Kenyatta, Kapteni Kung’u Muigai na Ngengi.
MAZISHI YA TOB COHEN KWA PICHA: Marehemu anazikwa katika makaburi ya Wayahudi kwenye barabara ya Wangari Maathai , Nairobi: mke wa marehemu ambaye ni mshukiwa wa mauaji hayo. #tobcohen #tukonews #KiswahiliAfrika
Picha: Nation, Zeckky Nemwel, Gukena FM Kenya pic.twitter.com/bxBcBsKKYN
— Tuko.co.ke (@Tuko_co_ke) September 24, 2019
Hata hivyo, dadake Cohen hakuhudhuria mazishi hayo. Hii ni baada ya yeye kurudi uholanzi siku moja baada ya Urathi wa Cohen kusomwa.
Mwili wa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 72 ulipatokana umetupwa kwenye tangi la maji lilokuwa ndani ya ua nyumbani kwake.