Kabogo awaonya magavana baada ya mwanasiasa kupata kichapo cha mbwa Ujerumani

Image result for william kabogo

Gavana wa zamani wa Kiambu, William Kabogo, ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotafuta huduma za matibabu nje ya nchi.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, gavana huyo wa zamani alichapisha video inayoonyesha makamu wa rais wa Seneti ya Nigeria akipewa kichapo cha mbwa na watu wake.

Mwanasiasa huyo alikuwa ameenda kutafuta matibabu huko Ujerumani.

Kwenye video iliyothibitishwa na Opera News mwanasiasa huyo anaonekana akipigwa na umati wenye hasira, wakati akiulizwa arudi nyumbani.

“Unataka utunzaji bora !!! Sisi pia tunautaka. Jenga hospitali ili kufaidi kila mtu. Hujaulizwa kuifanya kutoka mfukoni mwako, umejaza pesa kutoka kwa watu unaowaiba kila siku. Ifanye na pesa zilizopangwa. Mwishowe, tunakufa pamoja,” raia mwenye gadhabu alisema.

Kabogo aliwauliza magavana na waziri wa Afya, Sicily Kariuki, kuzingatia kile kilichotokea kwa mwanasiasa huyo wa Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *