Maisha yangu yamo hatarini- Betty Nambooze

Image result for Betty Nambooze Bakireke

Mbunge wa Munispaa ya Mukono, Betty Nambooze Bakireke, amemuandikia Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga akimfahamisha kuwa maisha yake yamo hatarini kutoka kwa watu wote wanaojulikana na wasiojulikana.

Nambooze alisema kuwa baada ya kufichua mianya katika usafirishaji wa kazi, amezidiwa nguvu na kuongezeka kwa vitisho kwenye maisha yake.

Hivi karibuni Nambooze alisababisha ghasia wakati akishutumu kampuni za usafirishaji wa wafanyikazi kwa kuuza wasichana wa Uganda kuwa watumwa.

Makampuni za kusafirisha wafanyikazi yalijitokeza na kupuuza madai hayo ya mbunge wa munispaa wa Mukono.

Nambooze alitoa maelezo hayo juu ya tishio kwa maisha yake wakati alipokuwa akikutana na wahasiriwa zaidi ya 50 wa usafirishaji wa kazi katika Nchi za Mashariki ya Kati kwenye Bunge.

Image result for speaker kadaga

Aliwaambia waandishi wa habari kuwa tangu hiyo siku amepokea vitisho kwa watu wanaomjua na wasiomjua ambayo imempelekeakutafuta usaidizi kwa Spika.

Alisema atafichua majina ya mawaziri wakuu wa serikali na wabunge ambao wanamiliki kampuni zinazohusika katika usafirishaji wa wafanyikazi wa ndani katika nchi za nje.

Alimhimiza spika kuanzisha haraka kamati teule ya kuchunguza madai hayo katika usafirishaji wa wafanyikazi wa ndani katika nchi za nje.

Baadhi ya wahasiriwa pia wameweka malalamiko kwa washauri wa nchi za waarabu kwa kuwalipa tena zaidi ya Shilingi milioni 50 kwa udanganyifu wa kuwasafirisha nje kwa kazi pamoja na kuajiri walinzi kuwanyanyasa.

Hapo awali Kadaga alikuwa na mkutano wa faragha na viongozi kutoka wizara ya Jinsia, Kazi na Maendeleo ya Jamii juu ya kuongezeka kwa udhalilishaji wa wafanyikazi wa ndani wa Uganda nje ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *