Sonko afichua jinsi Passaris alimvuja milioni kumi

Image result for SONKO AND PASSARIS

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amemrusha maneno makali kwa mwakilishi wa wanawake wa Nairobi Esther Pasaris.

Mike Sonko amethibitisha jinsi amekuwa akiwasiliana siku baada ya siku na Passaris kwa siku kama wanajaribu kutatua masuala yanayoathiri wakaazi wa Nairobi.

Related image

Sonko amesema kuwa Passaris amekuwa akiwasiliana naye mara kwa mara juu ya masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na jinsi ya kusaidia familia ambazo zimepoteza jamaa ndani ya Nairobi.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Jeff Koinange, Mike Sonko alionyesha baadhi ya ujumbe ambazo amekuwa akibadilisha na Passaris.

Cha kushangaza ni kuwa, Sonko alicheza sauti za Whatsapp za Passaris ambazo amekuwa akimtumia Gavana.

Hii inafuatia siku za hivi karibuni ambapo Passaris alimshutumu Sonko kwa kutomskiza na pia kutompata akiwa afisini au ata kwa simu.

Passaris anawapotosha Wakenya; Mimi huchukua simu zake. Alitoa mashtaka dhidi yangu na nilikuwa na haki ya kujibu, “alisema Sonko.

Hata hivyo, hakuweza kuucheza sauti iliyorekodiwa zaidi baada ya mkurugenzi wa habari wa Citizen Tv Monica Kiragu kutishia kukatisha mahojiano.

Image result for sonko and passaris

Sonko pia amedai kwamba Passaris alichukua milioni kumi wakati alikuwa na kesi ya Mahakama ambayo ilimshinikiza kwenye kiti ya ugavana.

Ninapopatia fedha za Esther Passaris, si fedha za rushwa, wakati ninapowapa watu masikini pesa, ni pesa za rushwa! Passaris amenivuja zaidi ya milioni kumi,” Sonko aliongezea.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *