Lissu atoka hospitali, afanya kampeni kwa njia ya WhatsApp;DC Jokate atinga gwanda, aanza na ‘operesheni Jokate’

Lissu atoka hospitali, afanya kampeni kwa njia ya WhatsApp

Moshi. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka hospitalini alipokuwa amelazwa kwa matibabu na baadaye kuhutubia mkutano wa kampeni za udiwani njia ya sauti akiwa nchini Ubelgiji. Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma Septemba 7 mwaka jana. Baada ya kujeruhiwa, mwanasiasa huyo alitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu na baadaye Januari 6 kuhamishiwa Ubelgiji. Akihutubia mkutano huo wa…Details<<

DC Jokate atinga gwanda, aanza na ‘operesheni Jokate’

DC wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na Kazimzumbwi wilayani humo kuondoka mara moja kabla hajatumia nguvu. Akiwa ndani ya msitu wa Ruvu Kusini Jokate amezindua operesheni ya siku 6 ya kuwaondoa wavamizi na kuipa jila la “Operesheni Jokate”. Jokate ameyafanya hayo leo Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako alienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya…Details<<

Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Akamatwa na Polisi Kwa Kujiunga na Kikundi cha Ukabaji

DODOMA: Jeshi la Polisi linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Itega, Mohamed Ramadhani(18) kwa kujiunga na kikundi cha uhalifu cha ‘Kamchape’ ambacho kinajihusisha na ukabaji – Kamanda wa Polisi, Gilles Muroto amesema kijana huyo amekuwa akijishughulisha na uhalifu ambapo kwa siku za hivi karibuni aliwahi kukiri kumkaba mama yake mzazi lakini mama huyo hakujua kuwa aliyemkaba ni mwanaye – Aidha, Kamanda Muroto amesema baada ya tukio hilo kijana huyo aliachiwa lakini…Details<<

Simba inawasha mitambo rasmi leo

Ikaja michuano ya Kombe la Kagame, wakaitesti tena mitambo yao kuona imekaaje. Kama zali wakafika fainali na kupoteza kwa Azam. Baada ya hapo mabosi wao wakaisafirisha timu masafar marefu hadi Ulaya na kuweka kambi nchini Uturuki. Kule wakajifua vya kutosha na leo Jumatano, Wekundu hao wataiwasha rasmi mitambo yao kwenye Uwanja wa Taifa. SIMBA ilitesti mitambo yake katika mechi ya SportPesa iliyofanyija Nakuru, Kenya. Kikosi kikafika fainali na kupoteza kwa Gor Mahia kwa mabao 2-0. Kuna watu wakacheka sana…Details<<

Ujumbe wa diamond kwa mwanawe Daylan siku yake ya kuzaliwa

Mwanamuziki Daimond leo amempa ujumbe mzito mtoto wake Daylan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa ambapo anatimiza mwaka mmoja. Kupitia ukrasa wake wa instagram daimond ameonyesha mahaba mazito mwanaye huyo na kumuandikia ujumbe huu “A Very Happy Birthday to the Next Platnumz…My Kitinda Mimba, Mswahili Mwenzangu, Maskini Mwenzangu…Mnyonge Mwenzangu…Mengi Uloyapitia Ukiwa mdogo, usiyejua hili wala lile yamenifanya nikupende sana na kuhakikisha nakulinda na kuku…Details<<

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *