Mwanasiasa mkongwe aliyewahi kuwa Mbunge wa Starehe Charles Rubia, amefariki.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na wakili wake, Seneta Irungu Kang’ata, Rubia alifariki akiwa na umri wa miaka 95 katika nyumba yake mtaa wa Karen jijini Nairobi.
VETERAN POLITICIAN Charles Rubia dies at his Karen home in Nairobi, his lawyer Senator Irungu Kangata confirms. pic.twitter.com/O2SdA7gI3H
— NationBreakingNews (@NationBreaking) December 23, 2019
Rubia alikuwa meya wa kwanza wa asili ya kiafrika wa jiji la Nairobi.
Baadaye, alichaguliwa kuwa mbunge na kisha kuteuliwa waziri.
Mnamo mwaka wa 1990, pamoja na hayati Kenneth Matiba, walikuwa mstari wa mbele wa kupigania mfumo wa vyama vingi vya kisiasa. alikamatwa na kutiwa mbaroni na aliyekuwa rais, Daniel Moi.
Aliachiliwa kutoka mbaroni baada ya mwaka mmoja na afya yake imekuwa katika hali mbaya tangu wakati huo.
Alikuwa mbunge wa Starehe kati 1969 hadi 1988.
Mnamo Juni, 2019, Rubia aliweka ombo la kulipwa fidia ya KSh 40 bilioni kutoka kwa serikali kufuatia mateso, kufungwa kinyume na sheria.