Mvua Kubwa Kunyesha Mikoa Hii leo Ijumaa 24 Machi

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la Mvua Kubwa inayotarajiwa kunyesha siku ya leo Ijumaa Machi 24 katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imeyataja maeneo ambayo mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuwa ni maeneo machache ya Mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora na Rukwa.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

TMA imeongeza kuwa, uwezekano wa mvua hizo kutokea ni wa wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *