Mvua Kubwa Kunyesha Mikoa Hii 11 Kesho Machi 14

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la Mvua Kubwa inayotarajiwa kunyesha siku ya Jumanne Machi 14 katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika maeneo machache ya Mkoa wa Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi,Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma na Ruvuma.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *