Mvua Kunyesha Mikoa Hii Kesho Jumapili Machi 5

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi nne katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, songwe, Iringa, Njombe, Mbeya, Mwanza, Kagera, Geita na Shinyanga.

Mikoa ya Singida na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, Dodoma, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Visiwa vya Unguja na Pemba, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Mbali na hayo, TMA imetoa angalizo la upepo mkali wa unaofika kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofika mita 2.0 katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani wa bahari ya hindi yanayojumuisha Mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Dar es Salaam na Visiwa bya Unguja na Pemba.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *