Waganda ni Wazembe, Rais Museveni Asema

Rais wa nchi ya Uganda Yoweri Museveni amewasuta wananchi wake na kuwataja kama watu wazembe mno.

Wakatu uo huo alisema kwamba nchini Uganda, hata watu wapumbavu wana uwezo wa kufaulu kimaisha kwa sababu hakuna haja ya kutia bidii katika shughuli za maisha yao.

Rais Museveni ametaja kuwa Waganda wana sifa hizo kwa sababu nchi hio imebarikiwa na mvua inayonyesha kwa misimu miwili hivo kuwafanya wazeembee katika shughuli nyingi haswa kilimo.

Alikuwa akiongea wakati wa mkutano na wanabiashara nchini Afrika Kusini ambapo rais wa taifa hilo Cyril Ramaphosa alihudhuria.

“Sisi (Waganda) tunayo misimu miwili ya mvua na hio ndio sababu Waganda ni wazembe kwani hali ya maisha sio ngumu kwao. Sio lazima ufanye kazi kwa bidi. Hata mpumbavu anaweza akaishi Uganda,” alisema Museveni kama alivyonukuliwa na chapisho la The East African.

Matamshi hayo ya Museveni yalionekana kuwashangaza wana

biashara wa Afrika Kusini na rais wao bwana Ramaphosa.

Chapisho hilo pia limesema Rais Museveni amekuwa akitoa matamshi hayo ya kuwadhalalisha Waganda mbele ya wapinzani wao wa  kibiashara.

Rais Museveni, 78, ameliongoza taifa la Uganda kwanzia 1986 na haoneshi dalili zozote za kung’atuka mamlakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *