Mvua Kunyesha mikoa Hii Kesho Machi 2

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi moja katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Dodoma, Singida, Ruvuma,  Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Mwanza, Mara Simiyu, Shinyanga, Geita, Rukwa, Songwe, Iringa, Njombe, Mbeya pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Mikoa ya Lindi na Mtwara, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Arusha, Kilimanjaro na Manyara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam,Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, na Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya juu vya joto tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *