Mvua Kunyesha Mikoa Hii Kesho Februari 28

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma,  Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Rukwa, Songwe, Iringa, Njombe, Mbeya pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua huku Mikoa ya Lindi na Mtwara ikitarajiwa kuwa na mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam, Visiwa vya Unguja na Pemba, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Kaskizini mwa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya juu vya joto tazama hapa chini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *