Utabiri wa Hali ya Hewa Saa 24 Zijazo

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia leo Februari 20 saa tatu usiku huu.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Kagera, Geita, Tabora, Kigoma, Katavi, Songwe, Njombe, Mbeya na Rukwa.

Mikoa ya Iringa, Ruvuma na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Maeneo mengine yaliyosalia nchini, ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro Kaskazini, Visiwa vya Unguja na Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Mtwara, Lindi na mengineyo yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto nchini tazama hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *