Halima Mdee Ampongeza Zitto

Mbunge Viti Maalum kutoka kambi ya Upinzani, Halima Mdee amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na chama chake kufuatia Mkutano wa kisiasa wa Chama hicho uliofanyika Leo Mbagala.

Kupitia Ukurasa wake wa Twitter, leo februari 19 Mdee aliandika ujumbe uliosomeka “Kaka zitto Kabwe Hongera sana kwa kazi ya leo pamoja na timu nzima ya ACT Wazalendo”

“Nawaona MBALI sana mkiendelea hivi. VYAMA MBADALA vina wajibu wa KUIBUA mabovu ya CHAMA TAWALA. Na kutoa MAJAWABU ya CHANGAMOTO za Wananchi. Havitarajiwi KULALAMIKA tu. Big up Bro!!” Aliandika Mdee.

Naye Zitto, alitoa shukrani kwa pongezi hizo na kuahidi kujenga Chama cha Siasa ambacho ni mbadala wa uhakika.

Aliongeza kuwa, wazo la Taifa la wote maslahi kwa wote,  litabadili kabisa namna siasa hapa nchini Tanzania inavofanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *