TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa, Upepo Mkali Maeneo Haya

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) leo Februari 10, imetoa angalizo la kuwepo kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

TMA imezitaja athari zinazoweza kutokea kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na kuathirika kwa shughuli za kiuchumi na usafirishaji hivyo wananchi wazingatie na kujiandaa.

Katika hatua nyingine, TMA imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilometa 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia Mita mbili katika maeneo ya Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Kwingine ni baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kaskazini (Tanga) na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *