Taarifa ya Hali ya Watanzania Waishio Uturuki

Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Luteni Jenerali Yacoub Mohamed ameeleza hali ilivyo nchini humo baada ya tetemeko la ardhi kutokea siku chache zilizopita na kusababisha maafa makubwa pamoja na vifo vya watu.

Akizungumza katika Supa Breakfast ya East Africa Radio leo Februari 9, Balozi Yacouba amesema mpaka sasa hawana taarifa ya mtanzania yeyote aliyefariki wala kujerujiwa katika miji sita waliyowasiliana nayo.

“Watanzania waliokuwa wanaishi katika miji kumi iliyoathirika ubalozi umefanikiwa kuongea nao katika miji sita na tunaendelea kuangalia katika miji mingine minne kama kuna watanzania wanaishi huko.” Alifafanua Balozi Yacoub

Kuhusu hali ya uokoaji amesema zoezo hilo limekumbwa na changamoto ya hali ya hewa kwani kuna baridi kali ,na theluji imeanza kuanguka na miundombinu imeharibika hivyo kuleta changamoto ya kuweza kufika kutoa msaada na uokoaji.

Balozi Yacoub amewashauri wazazi ambao mapaka sasa hawajawasiliana na ndugu zao kuwasiliana na ubalozi moja kwa moja.

Aidha ameeleza kuwa, wanaotaka kuondoka katika maeneo yaliyoathirika Turkish Airlines imetoa mpaka tarehe 13 kuondoka katika hayo maeneo na safari za ndege zipo kwenye yale maeneo ambayo hayajaathirika, shughuli zinaendelea kama kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *