TMA Yatoa Tahadhari Mvua Maeneo Haya

Mamalaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia usiku huu tarehe 7 Februari.

Utabiri huo umetaja maeneo yatakayokua na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Manyara.

Kwingine ni Mikoa ya Pwani ikijumuishwa na Mafia, Visiwa vya Unguja na Pemba, Mkoa wa Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Mara, Tabora, Kigoma, Katavi, Songwe, Rukwa, Mbeya na Iringa.

Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Njombe, Ruvuma, Mtwara na Lindi nayo inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo  katika maeneo machache pamoja na vipindi vifupi vya jua.

Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na Mvua nyepesi katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Kwa viwango vya joto vinavyotarajiwa nchini tazama hapa chini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *