Tumia Mtandao Bila Malipo Kupitia Ushirikiano wa Opera na Safaricom Nchini Kenya!

Jambo Kenya!

Tunafurahia kutangaza kuwa tumeshirikiana na Safaricom ili kukupatia 50 MB za bure kila siku unapotumia Opera Mini, Opera News na Opera News Lite kwa simu yako kwenye mtandao wa Safaricom.

Hii yamaanisha kwamba utaweza kuokoa pesa na data unapotumia mtandao bila malipo kupitia Opera Mini, Opera News and Opera News Lite.

Kama watumia Safaricom nchini Kenya, na tayari uko na mojawapo ya apps hizi tatu, uko tayari kuanza kufurahia matumizi ya mitandao bila kutumia data. Unapopata 50 MB kila siku kwa Opera Mini bila malipo, utasalia na data za ziada za kutazama picha kwenye Instagram na kujulia marafiki wako hali kwenye mtandao wa Facebook. Haya yote yawezekana ukijiunga na mitandao hizi za kijamii kupitia Opera Mini.

Kwa 50 MB kila siku bila malipo, waeza kusoma habari moto moto punde zinapochipuka na matukio mengine yanayofanyika karibu nawe kwenye Opera News na Opera News Lite.

Tumia mtandao kwa mwendo wa kasi mara nne zaidi

Opera Mini ni programu ndogo lakini yenye nguvu mno inayotumika kupekua mitandao kwenye simu ya mkono. Programu hii ina vipengele kama vya kupunguza matumizi ya data, kushiriki nakala bila mtandao, na  kuzuia matangazo ya kibiashara.

Mapema mwaka huu pia tulitangaza kusimikwa kwa vyombo vyetu katika vituo vya data vya Opera jijini Mombasa. Hatua hii iliwezesha kupunguza muda unoatumika kupakua nakala mitandaoni na kukuwezesha kupekua mitandao kwa kasi mara nne zaidi. Hii yakuwezesha kufurahia matumizi ya mitandao ya haraka kuliko programu zingine zinazopatikana mitandaoni ama zilizosindikwa kwa simu yako.

Hifadhi data zaidi

Kama unavyofahamu, Opera Mini ina uwezo wa kuhifadhi data yako kupitia vipengele vyake vya kipekee. Unapowezesha uhifadhi wa data kwenye Opera Mini, programu hii yaweza kukuokolea hadi 80% ya data zako. Hii ni kwa sababu vipengele vya kuokoa na kuhifadhi data vinauwezo wa kupunguza kiasi cha data inayotumika kupakua nakala kwenye simu yako.

Habari za hivi punde kuhusu COVID-19

Opera yakusudia kukufahamisha vilivyo kufuatia kuenea kwa kwa visa vya coronavirus barani Afrika. Kwa hivyo, hivi majuzi tuliongeza kipengele cha kukuwezesha kupata taarifa rasmi kutoka kwa serikali na wizara ya afya kuhusu COVID-19 kwenye Opera Mini.

Kipengele hiki kiko kwenye ukurasa wa kwanza wa Opera Mini. Mara tu unapokibonyeza, utapata taarifa rasmi kuhusu visa vya COVID-19 nchini Kenya, mapendekezo ya jinsi ya kuzuia maambukizi, na taarifa kuhusu mikakati ambayo serikali imechukua kuzuia kusambaa kwa virusi hivi.

Soma habari bila malipo

 Hadi sasa, Mei 2020, Opera News na Opera News Lite ziko miongoni mwa apps za habari zilizopakuliwa zaidi nchini Kenya kulikanga na ripoti ya AppAnnie.

Opera News hutumia mfumo wa AI ambao unaiwezesha kusambaza nakala zilizobinafsishiwa wasomaji kuhusu habari kuu, video moto moto na vitengo vingine zaidi ya arubaini.

Opera News Lite, ni toleo nyepesi ya programu ya Opera News. App hii imeundiwa vifaa ambavyo havina nafasi kubwa ya kuhifadhi nakala na vinaweza kupakua chini ya 1GB pekee. Opera News Lite pia ni bora kwa wenye mitandao yenye kasi cha chini kwani ni sikivu na hutumia data kidogo sana kupakua nakala kwa haraka.

Je, nimehitimu kutumia mitandao bila malipo?

50 MB za kila siku bila malipo zapatikana unapotumia app zetu tatu. Kwenye Opera Mini, waweza kupekua mitandao bila malipo ukitumuia toleo la mwisho kabisa la app hiyo. Kwa hivyo, ili kupekua mtandao bila malipo, hakikisha umesimika toleo jipya la Opera Mini kupitia hatua hizi:

Enda kwa “Opera Mini > Settings > About Opera Mini > Check for Update”

Hongera! Sasa uko tayari kutumia mitandao bila malipo kupitia ushirikiano huu wa Oprea na Safaricom. Ni vipengele vipi vya Opera Mini unavyovipenda sana? Ni vitengo vipi vya habari vinavyokufurahisha? Tuambie kwenye sehemu ya maoni. Ni furaha kwetu kusikia kutoka kwako.

Uko na swali lolote? Wasiliana nasi kupitia akaunti zetu kwenye mitandao ya kijamii ambapo pia tutachapisha maelezo zaidi kuhusu huduma hii. Kumbuka, hakikisha umetumia Opera Mini na kusoma habari kwenye Opera News ama Opera News Lite ili kupata 50MB bila malipo kila siku!

Maswali ya Mara Kwa Mara:

Mpango wa data bila malipo wamaanisha nini haswa?

Kama watumia mtandao wa Safaricom, waweza kutumia mitandao na kusoma habari kupitia Opera Mini, Opera News na Opera News Lite bila malipo. Utapata 50MB ya matumizi bila malipo kila siku.

Je, nimehitimu kupata 50MB bila malipo?

Mpango huu ni kwa yeyote anayetumia Opera Mini, Opera News na Opera News Lite kwenye mtandao wa Safaricom. Watumiaji wapya watajiunga na mpango huu moja kwa moja.

Nitapataje data bila malipo kupitia Opera Mini, Opera News na Opera News Lite?

Kama tarayi watumia Opera Mini, Opera News au Opera News Lite, utapata 50MB za bure kila siku za kutumia kwenye app hizi. Unachohitajika kufanya ni kufungua tu app na kufurahia muda wako mtandaoni. Utapata ujumbe wenye maelezo zaidi kuhusu matumizi yako ya data na mpango huu kwenye app.

Nitatumiaje hizi 50MB za bure?

Data za bure ni za kupekua mitandao pekee. Mpango huu hajumuishi kutazama video wala kapakua nakala kutoka kwenye mitandao – data zako za kawaida zitatumika kwa huduma hizi. Usiwe na shaka, mpango wa kupekua mitandao bila malipo utakuwezesha utakuwezesha kufungua tovuti kadhaa na kusoma habari kwenye Opera Mini, Opera News na Opera News Lite.

Mpango huu unatumika kwenye app zingine za Opera?

Hapana. Mpango huu unatumika kwenye Opera Mini, Opera News na Opera News Lite pekee.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *