Mwanamuziki Papa Dennis Apatwa Amefariki Barabarani

Mwili wa Papa Dennis Umepatikana barabarani huko Pangani, Nairobi usiku wa Ijumaa, Februari 7 kama ilivyoripotiwa na K24 Digital.

Kifo chake kilithibitishwa na kuchapishwa na msanii wa injili Daddy Owen ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio.

Alipatikana amekufa kando ya barabara karibu na makao makuu ya Chama cha Jubilee,” Daddy Owen alifahamisha.
Walakini, Kilichosababisha kifo cha Papa Dennis bado hakijajulikana wazi.

Image may contain: 1 person, smiling

Anajulikana kwa mtindo wake wa maisha ya hali ya juu na mtindo wa mavazi yake. Papa Dennis alishinda tuzo kadhaa katika kazi yake kama vile Tuzo za Mwafaka za mwaka wa 2015, 2016 na 2017, Tuzo za Video za Muziki za Kiafrika za 2018 (AFRIMMA), na tuzo ya Msanii Mpendwa ya 2019.

Bado hakujaeleweka kama alijitoa uhai kwa kuruka kutoka jengo hilo au aligongwa na gari. Wanamuziki wengine waliofika kwenye tukio ni kama vile Ringtone, Daddy Owen na wengine.

Mola ailaze Roho yake Pema Peponi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *