James Nyoro aapishwa kuwa Gavana mpya wa Kiambu

Aliyekuwa Naibu wa Gavana wa kaunti ya Kiambu, James Nyoro ameapishwa rasmi kuchukua nafasi ya gavana wa Kiambu Ijumaa, 31, Januari.

Hatua hii inajiri siku mbili baadaya aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Ferdinand Waititu kungatuliwa mamlakani na bunge la seneti.
Hafla ya kuapishwa kwa Nyoro iliongozwa na jaji John Onyiego akisadiana na katibu wa kaunti hiyo Martin Mbugua.

Kulingana na sheria, Naibu gavana huridhi nafasi ya gavana anapotimuliwa mamlakani.

Chama cha Jubilee kilichua nafasi ya kwanza katika kumpa kongele gavana Nyoro baada ya kuapishwa na kuchukua hatamu.

Waititu alitimuliwa mamlakani kufuatia kashfa ya ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya ya mamlaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *