Mtihani wa KCSE 2019 Watangazwa

Image result for magoha kcse 2019

Matokeo ya mitihani ya KCSE ya 2019 yametolewa.

Waziri wa Elimu, George Magoha, Jumatano amezindua matokeo ya mtihani huo ambao ulifanywa na wanafunzi 699,745 nchini kwenye jumba la Mtihani house.

Mwanafunzi bora wa KCSE mwaka huu ni Buluma Tony 87.159, akifuatiwa na Barasa Maryann Njeri 87.087, AbogeDavid Odhiambo 87.080. Anthony Awuor 87.00 Natasha Wawira, 86.961, Kizito Ezra, 86.960, Hellen Njoki 86.914, Siele Chelangat 86.900, na Laura Chelangat Ruto 86.56.

Kulingana na waziri Magoha, wizara yake imejaribu juu chini kukabiliana na wizi wa mtihani, jambo ambalo wamefaulu.

Hata hivyo, mtihani huu ulikumbwa na changa moto nyingi baada ya usahihisaji kusitishwa kwa muda baada ya waalimu kulalamikia malipo na mazingira duni ya senta waliokuwa wakifanyia shughuli hiyo.

Kaunti za Kisii na Migori zilirekodi idadi kubwa ya makosa dhidi ya kanuni za mtihani huo  ulioanza mnamo  Novemba 4 hadi Novemba 27.

Image result for kcse 2019

Watahiniwa watatu walifariki wakati wa mitihani, kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KNEC, Mercy Karogo alieleza Jumatano.

Zaidi ya hayo, watahiniwa kadhaa waliugua katika kipindi hicho. Mmoja wa watahiniwa hao alilazwa baada kuikaribia kemikali yenye sumu (Xylene) wakati wa mtihani wa karatasi ya Kemia, tukio ambalo serikali ilikataa kabisa.

Mnamo 2018, Juliet Owino kutoka Pangani Girls aliibuka mtahiniwa bora zaidi katika mtihani wa KCSE. Kupata Matokeo kwenye sumu yako, tuma nambari ya usajili kwenye 20076.

Maelezo zaidi kufutia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *