Ajali ya Asubuhi Kuwaangamiza Watu Watano na Kuacha Majeruhi 62

Watu watano wamefariki na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili ya kusafiria ya kisasa kugongana huko Kiongwani kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi, Kamanda wa Polisi wa Kata ya Makueni Joseph ole Napeiyan amesema.

Waliojeruhiwa katika ajali hii ya kuamkia leo saa 2.40 walikimbizwa katika Hospitali ya Kaunti ndogo ya Sultan Hamud kwa matibabu.

Polisi wa trafiki walikimbia katika eneo la tukio kuzuia msukumano wa magari.

“Moja ya basi hizo ilikuwa inatoka mji wa Malaba wakati ile nyingine ilikuwa ikielekea Nairobi wakati ajali ikitokea. Basi lililokuwa likitoka Mombasa lilipoteza mwendo na kugongana na basi linalokuja,” alisema Bw Ole Napeiyan.
Ajali hio ilitokea kwenye eneo la hatari ambalo limerekodi zaidi ya ajali kumi za barabarani katika wiki tatu zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *