Gavana Sonko Atiwa Ndani Tena Kwa Siku Mbili Zaidi

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atakaa siku mbili zaidi katika ulinzi wa polisi akisubiri uamuzi wa dhamana Jumatano.

Atazuiliwa katika Gereza la Industrial Area Remand Prison kwa siku mbili zaidi.

Sonko Jumatatu alifikishwa mbele ya hakimu mkuu Douglas Ogoti katika Korti ya Sheria ya Milimani ambapo alikana makosa zaidi ya 30 katika kesi ya ufujaji wa pesa takriban Ksh357 milioni.

Upande wa mashtaka, ukiongozwa na James Kihara, uliimarisha msimamo wake Sonko kupinga ombi lake la dhamana kwa kudai kuwa amewatishia maafisa wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) wakati wa uchunguzi. Na kwamba ana uwezo wa kutoroka nchini.

Waendesha mashtaka wanaoshughulikia kesi yake pia waliiambia korti ya hakimu kwamba Sonko ana kesi ya jinai inayosubiriwa “kwa sababu amekataa kujiwasilisha.”

Tayari, upande wa mashtaka umesema hati ya kukamatwa imetolewa na korti ya Hakimu Mkazi huko Mombasa.

Kwa hivyo, upande wa mashtaka ulisema kwamba ikiwa ataachiliwa kwa dhamana, “Sonko anaweza kuondoka au kuwatishia mashahidi.”

Mwendesha mashtaka alitafuta pia maagizo ya kumzuia Sonko na maafisa wengine wa umma kurudi katika ofisi zao wakisubiri kusikilizwa na uamuzi wa kesi hizo, kuwazuia watuhumiwa kuwasiliana, kuwatisha mashahidi na wachunguzi na, pasi za kusafiria na mahakama.

Sonko alikamatwa Ijumaa saa nane mchana kwenye kizuizi cha barabara huko Voi baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kutoa hati ya kukamatwa kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *