Rais Mustaafu Moi Alazwa Hospitalini Tena

President Uhuru with former President Daniel Arap Moi at his Kabarnet Gardens residence in Nairobi during a past meeting.

Rais mustaafu Daniel arap Moi amelazwa tena siku mbili baada ya kuachiliwa baada kupata nafuu.

Kulingana na ripoti mbalimbali, Moi amelazwa katika hospitali ya Nairobi Hospital.

Msemaji wa Moi, Lee Njiru ameliambia gazeti la The Star kuwa rais mstaafu alilazwa hospitalini Jumamosi asubuhi.

Si bayana iwapo Moi alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa walio hali mahututi au kwenye wadi ya jumla ya watu mashuhuri.

“Alirudishwa lakini haijulikani ni wadi ipi alipolazwa. Walinzi wake wameonekana kote na wanafamilia yake pia wameonekana,” mmoja wa walio na habari aliambia The Star.

Mnenaji wa Moi, ambaye anaishi Nakuru, amekanusha kujua iwapo rais huyo wa zamani alikuwa amelazwa hospitalini.

“Sina uhakika, lakini nitadhibitisha na kisha kuwajulisha,” Njiru alisema.

Njiru alitangaza Alhamisi wiki iliyopita kuwa Mzee Moi alikuwa ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kupata nafuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *