Babu Owino Akimbizwa Hospitali Baada ya Kuugua

Mbunge wa Embakasi Mashariki Paul Ongili alias Babu Owino Jumapili, Novemba 3, alituma picha yake akipata matibabu hospitalini.

Mbunge huyu amekuwa akiugua kwa muda wa wiki moja iliyopita na alikuwa hospitalini juu ya ugonjwa ambao haujulikani.
Image result for BABU OWINO
Alishiriki picha akiwa amelazwa katika kitengo cha radiology akisubiri matibabu.
“Mungu aniponye kwa sababu lazima niongoze taifa hili siku moja,” alisema kupitia Facebook yake.
Haijabainika wazi ni lini mbunge huyo alianza kuugua lakini upekuzi wetu unaonyesha amekuwa nje ya uwezo kwa sababu hiyo hiyo, akakosa kampeni muhimu za Kibra kwa mgombea wa ODM Benard ‘Imran’ Okoth.
Picha ya Babu Owino akipokea matibabu kwenye mashine za hospitali imechipuka kwenye mtandao. Picha: Babu Owino Source: Facebook
Babu ambaye alizungumza na Wakenya.co.ke siku ya Alhamisi, Oktoba 31 alifunguka kuwa alikuwa hospitalini akipokea matibabu akishindwa kutaja kile alikuwa akiugua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *