Ajali: Magari ya Rundikana Kwenye Barabara Kuu ya Thika

PHOTOS: Thika Road accident near Muthaiga Police Station

Zaidi ya magari sita yanaripotiwa kuhusika kwenye ajali katika barabara kuu ya Thika karibu na Kituo cha Polisi cha Muthaiga.

Mabasi manne na magari ya uchukuzi ni miongoni mwa magari ambayo yaligongana kukikucha leo. Inaripotiwa kuwa Basi la kampuni ya Virginia, lilikosa mwelekeo na kuteleza hadi nje ya barabara na kugonga reli ya walinzi kufuatia mvua kubwa ilionyesha.

Walioshuhudia ajli hio walisema kuwa basi hilo lilikuwa kwenye harakati ya kujipisha mbele ya lingine wakati dereva aliposhindwa kulidhibiti.

Kutokana na mwonekano duni, magari yaliyokuwa nyuma yanaripotiwa kugongana na mabasi hayo mawili kisha kusimama katikati ya barabara.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara hiyo kuu.

Polisi walipitia wakati mgumu kuelekeza trafiki kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha huku madereva wengine wakipunguza mwendo ili kushuhudia kisa hicho.

Madereva walioelekea Ngara walilazimika kutumia njia mbadala.

“Bora kutumia njia ya huduma kutoka Muthaiga. Thika Rd imefungwa kabisa, ” Kinyanjui Kombani alisema kwenye Twitter.

Madereva wamehimizwa kutumia tahadhari barabarani huku msimu wa mvua ukianza.

“Mvua zinatarajiwa kuongezeka na zaidi ya 40milimita kutoka Alhamisi, Oktoba 17 hadi Jumapili, Oktoba 20 katika mikoa ya Pwani, Kusini mwa Mashariki, Kaskazini Mashariki, Magharibi na Mkoa wa Kati pamoja na eneo la Nairobi,” Idara ya hali ya hewa ya Kenya ilisema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *