Mwanahabari wa KTN Tony Gachoka Akamatwa

Image result for tony gachoka
Mwanahabari Tony Gachoka

Mtangazaji wa kipindi maarufu cha KTN Tony Gachoka amekamatwa huko uwanja wa ndege wa Diani, kaunti ya Kwale.

Ripoti za polisi zilionyesha kwamba mwendesha kipindi cha Point Blank alikamatwa kwa kusababisha usumbufu akiwa mlevi baada ya kuzuiliwa kutoka kwa kupanda ndege.

Mkuu wa polisi wa Msambweni Nehemia Bitok ambaye alithibitisha jambo hilo, alifafanua kwamba Gachoka alizuiliwa kuingia kwenye ndege ya Silverstone iliyokuwa ikielekea jijini Nairobi kutokana na kuwa na vinywaji vyenye vileo.

Washahidi walielezea kuwa mwanahabari huyo alisisitiza kusafiri na bidhaa hizo licha ya sheria iliyowekwa kwenye uwanja wa ndege hiyo.

Habari zaidi zinasema kuwa maji yalizidi unga wakati Gachoka aliposababisha ghasia na kupelekea kuwadhulumu abiria wengine.

Mfanyikazi huyo wa zamani wa Raila Odinga anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Diani.

Bitok ameongeza kuwa Gachoka atafikishwa kortini Alhamisi na kushtakiwa kwa kusababisha usumbufu na ulevi sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *