Rekodi ya Sauti Baina ya Sonko na Mwandani Yaweka Wazi Uozo Ndani ya Kaunti ya Nairobi

Rekodi ya sauti kati Gavana Sonko na Jamaa mmoja imevuja na kuweka wazi uozo ulioko ndani ya Jumba la City Hall.

Gavana huyo na mwandani wake waliongelea  maswala kadhaa yanayohusu jiji la Nairobi na hata kuwashambulia viongozi kadhaa ndani ya kaunti.

Sonko, ambaye alikuwa akizungumza na mtu ambaye alikuwa amemsajili kama Simo, alipokea habari nyingi ambazo ziligusa sekta mbali mbali ndani ya kaunti.

Kwanza, gavana ambaye alikuwa nchini Ufaransa wakati huo, aliarifiwa kuwa Spika wa Kaunti Beatrice Elachi alikuwa amealikwa kwa mkutano na mbunge mteule Maina Kamanda, lakini alionyesha uaminifu wake kwa Sonko kwa kuwadharau wale waliomuita.

Katika usemi wake, Sonko aliendelea kumtukana Kamanda na kudai kuwa alijua kuwa mbunge huyo wa zamani wa Starehe alikuwa amenyakua viwanja kadhaa huko Eastleigh na alikuwa amewafeli watu wa Nairobi wakati wa enzi ya Rais mstaafu Mwai Kibaki.

Aliahidi kufuatilia suala hilo hadi pale Kamanda atakapolipa yote aliyokuwa amenyakua kutoka kwa wakaazi wa Nairobi.

Simo alimfahamisha gavana kwamba mkutano huo ulihudhuriwa pia na Kiongozi Mkuu wa Nairobi Abdi Guyo, Waithera anayejulikana na gavana na Kadoz.

Alifahamishwa zaidi kwamba Guyo na waandani wake walikuwa wamenunua fimbo za mbao ambazo walikuwa wakibeba kwenye magari yao

Simo alifunguka zaidi kwamba tayari alikuwa amewasiliana na bosi wa flying squad Musa Yego ambaye sasa alikuwa akiyatafuta magari ya Guyo.

Katika mazungumzo hayo ya kupigia simu, jasusi huyo alionekana kumpa repoti gavana matakwa yake kumnyatua Guyo kama kiongozi mkuu wa Jubilee kwenye Bunge la Kaunti ya Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *