Wakenya Washambulia Harambee Stars kwa Kuharibu Sherehe

Image

Wakenya wenye mori waliwasha moto kwenye mitandao ya kijamii na kuelekeza hasira yao kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu, Harambee Stars. Wakenya hao walidai kuwa wachezaji hao walijaribu kuharibu wikendi iliyojaa sherehe katika nyanja ya michezo.

Stars walipewa kichapo katika mechi ya kirafiki kati ya kenya na msumbiji. Hii ilikuwa mechi yao ya pili ya Kirafiki chini ya usuka wa kocha wao mpya Francis Kimanzi. Mechi hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kasarani mnamo Oktoba 13

Kichapo cha Kenya kilikuja siku moja tu baada ya Eliud Kipchoge kufanya historia huko Vienna, Austria, kwenye mbio ya INEOS 1:59, ambapo aliandikisha saa ya 1: 59: 40.02, na kuwa mtu wa kwanza duniani kukimbia mbio hizo chini ya masaa mawili.

Sherehe hizo ziliendelea Jumapili, baada ya Brigid Kosgei kuvunja rekodi ya dunia katika mdio za kilomita 42. Aliivunja rekodi ya Paula Radcliffe kwa sekunde 81 na Kuandisha ushindi wa Chicago Marathon.

Hii hapa baadhi ya maoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *