Matiangi Atangaza Alhamisi kama Likizo ya Umma

Interior CS Fred Matiang’i during a past function

Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiangi ametangaza kuwa Alhamisi itaorodheshwa kama likizo ya umma.

Kupitia kwenye gazeti, Matiangi ametangaza siku hiyo itazingatiwa kama siku ya Moi.

 

Uamuzi huo unakuja baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi mnamo 2017 kwamba siku ambayo ilikuwa imetolewa, ikubaliwe tena na serikali.

Jaji Odunga alisema kufutwa kwa likizo hiyo ni ukiukaji wa Sheria ya Likizo ya Umma.

“Kwa hivyo ninatoa tamko kwamba kutolewa kwa siku ya 10 ya Oktoba kutunzwa kama likizo ya umma ni ukiukaji wa sheria na ni kinyume cha kifungu cha 2 (1) kama inavyosomwa na sehemu ya 1 ya ratiba ya Sheria ya Likizo ya Umma.”

Jaji hata hivyo alisema kwamba kulikuwa na njia ya kisheria ya kuondoa siku kama ilivyo kwa katiba.

“Isipokuwa na mpaka bunge litakaporekebisha Ratiba ya 1 ya Sheria hiyo au waziri atabadilisha hiyo tarehe nyingine, tarehe 10 Oktoba katika kila mwaka itaendelea kuwa likizo ya umma.” Alielezea jaji.

Uamuzi wa Odunga ulitokana na maombi ambayo yalifikishwa na Gregory Nyauchi ambaye alipeleka malalamiko kortini kupinga hoja hiyo ya kuacha kuadhimisha siku hiyo.

Nyauchi alisema kuwa kuachana na likizo hiyo kulinyima wafanyikazi haki yao kama ilivyoainishwa na sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *