Mpigambizi wa Kibinafsi Ajiondoa kwenye Shughuli za Uokoaji Likoni

Image result for likoni ferry accident today

Janga la Likoni limeendelea kupokea vikwazo zaidi baada ya kuibuka  kuwa mpigambizi wa kibinafsi ialiyekuwa ameajiliwa na familia anasimamishwa kazi.

Mpigambizi huyo alisitishwa kwa madai kuwa alikuwa akiipa familia hiyo habari ya uwongo kuhusu eneo la miili hiyo miwili ambayo iliingia kwenye Bahari la Hindi.

“Acha nibaki kando, niruhusu niende. Sitasema chochote kwa sababu kuna ubishani …” aliwaambia wanahabari huku akiondoka Likoni.

Huduma za Feri za Kenya Jumatano walisema kwamba walikuwa wamezingundua sehemu 14 ambazo gari iliyozama ilikuwa na uwezekano wa kuwemo. Tayari walikuwa wamekagua maeneo tano kati ya yale 14.

Kikosi cha uokoaji tayari kilikuwa kimeziachilia roboti chini ya maji pamoja na kamera za kusaidia katika kutafuta gari.

“Wizara inajali, serikali yote inahusika na kuweka hatua kuhakikisha kuwa uokoaji huu unakamilika haraka iwezekanavyo,” Katibu mkuu wa Wizara ya Usafiri Esther Koimett alisema

Operesheni ya uokoaji inatarajiwa kuendelea hadi gari na mabaki ya dereva na abiria yatakapopatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *