Jengo Laporomoka Kakamega, Idadi ya Watu Walioathirika Haijulikani

Jengo ambalo halijakamilika leo hii limeporomoka huko Butali, Kaunti ya Kakamega . Inasemekana kuwa wafanfyikazi waliokuwa wakifanya kazi kule wametekwa ndani.

Ripoti isiyo na uthibitisho inaonyesha kwamba mtu mmoja ameangamia katika tukio hilo la leo asubuhi. Sababisho la tukio hilo bado halijulikani.

Walakini, Wakazi wanasema kuwa ujenzi ulikuwa unaendelea kwenye sehemu hiyo wakati ukuta uliporomoka. Jengo hilo linasemekana kuwa la kibinafsi, lenye ghorofa moja iliyojengwa.

Hii, inakuja wiki chache baada ya shule ya Precious Talent iliyoko Dagoretti kuporomoka na kuwaangamiza wanafunzi nane.

Maelezo zaidi kufuatia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *