Maneno ya Mwisho ya mhasiriwa wa janga la Feri kwa Mumewe

John Wambua mume wa Mariam Kighenda, mama ambaye alikufa baada ya gari lake kupoteza mwelekeo kwa meli na kuingia Bahari la Hindi siku ya Jumapili, Septemba 29, ameelezea habari ya mawasiliano yake ya mwisho na mkewe.

Akiongea na waandishi wa habari kutoka Daily Nation, alisema kuwa mkewe alikuwa anatoka kwenye shamba la familia huko Msambweni, kaunti ya Kwale.

“Mke wangu alikuwa ameenda kutafuta mboga kama yeye hufanya mwishoni mwa wiki.

“Alipiga simu alipofika kwenye kivuko na nilijua atarudi nyumbani hivi karibuni,” Wambua alikumbuka huku machozi yakimtoka.

Mariam Kigenda and her daughter Amanda Mutheu. Their vehicle rolled and plunged into the Indian Ocean while the ferry was midstream.

Aliposikia habari mbaya kwa mtandao wa kijamii alijaribu kuwasiliana na mkewe lakini majaribio yake hayakuzaa matunda.

“Mara moja nilijaribu kumpigia simu lakini sikumpata, nimeumia moyo. Nitaanza wapi? ”Aliongea kabla ya kububujikwa na machozi.

“Hakuna kinachoendelea. Hakuna anayeonekana kumjali dada yangu na mpwa wangu. Hakukuwa na mtu wa kuokoa maisha yake na hakuna mtu anayetaka kusaidia kutoa miili hiyo.

“Familia haijapata neno kutoka kwa jeshi la wanamaji [wala] Huduma za Feri za Kenya hata imechukua uamuzi wa kuwalipa watu mbali mbali kutafuta miili ya Kighenda na binti yake,” dadake Miriam alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *