Wanafunzi wa Precious Talent Wapuuza Agizo la Magoha

Magoha

Wanafunzi wa Shule ya Precious Talent wamelipuuza agizo la Waziri wa Elimu George Magoha kuhamia shule mpya Jumatatu, Septemba 30.

Kulingana na Magoha , takriban ya wanafunzi 90 kati ya 480 waliripoti shule zao mpya asubuhi ya leo. Wanafunzi walitakiwa kuripoti kwa shule za msingi za Jamhuri, Ngong Forest na Riruta Satelite lakini ni wanafunzi 69 , 20 na chini ya 10 mtawalia waliaripoti kwenye shule hizo.

“Kwa wakati huu, serikali imeongeza uwezo zaidi katika Shule ya Ngong Forest ambayo ni bora na iko karibu na makwao,” aliongeza.

Wanafunzi wengi, hata hivyo, walipendelea kujiunga na shule ya Jamhuri ambayo kwa mujibu wa Magoha ni mbali zaidi kuliko shule ya Ngong Forest kwa umbali.

Magoha pia alifafanua kuwa wazazi walikuwa wametembelea shule ya Ngong Forest kukagua iwapo ilifikia viwango vyao.

Walakini, wazazi walikuwa na uhuru wa kuhamisha watoto wao kwa shule walizopendelea na sio lazima wapeleke katika shule hizo tatu.

A section of Ngong Forest Primary School that was to recieve pupils from Precious Talent school. It is one of the three schools CS George Magoha recommended for the transfer.Madarasa katika shule ya Ngong Forest ambapo walitengewa wanafunzi wa Precious Talent

Mnamo Jumatatu, Septemba 23, Magoha alitangaza kufungwa kwa siku 4 kwa Shule ya  Precious Talents. Baadaye aliamuru wanafunzi wa shule hiyo kusambazwa kwa shule za umma baada ya mmiliki wa shule hiyo kukamatwa.

Siku ya Jumatano, Septemba 25, Magoha aliifunga shule ya msingi ya St. Catherine Bombolulu na kuamuru kuhamishwa kwa wanafunzi 207 katika shule ya jirani, Ayany Estate Primary.

Kulingana na Waziri, Shule ya Msingi ya Bombolulu ilikuwa katika hali sawa na ile ya shule ya Precious Talent huko Ng’ando Dagoretti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *