Wahuni Washambulia Eneo la Kitui Katika Mzozo wa Kikabila

Hali ya taharuki imetanda eneo la Kitui baada ya majambazi wanaoshukiwa kuwa wa asili ya kisomalia kushambulia kijiji mashariki ya kaunti hiyo na kumuua mfanyabiashara wa eneo hilo.

“Nimesikitishwa sana na nimefadhaika kwa shambulio la mahuni kwenye njia panda ya Muthumulani ambayo iko kwenye barabara ya Engamba na Twambui ya Endau, Kitui Mashariki ambapo tumempoteza mfanyi biashara Bwana Kitonga Musembi. Wazimu huu lazima ukome,”   taarifa rasmi ya gavana ilisoma.

Ngilu aliomba vyombo vya usalama za kitaifa na za mitaa kushughulika kwa haraka na kuchunguza suala hilo na kuwakamata wahusika.

” Mkutano wetu ujao na waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt Fred Matiang’i na vyombo vya usalama nchini  unakusudia kushughulikia mzozo huu wa zamani ambao umewaacha watu wetu wakiwa na majeruha, kutengwa na kufa kwa kushambuliwa bila huruma na majambazi hawa,” alifunguka.

Aliendelea kuomboleza na familia ya mfiwa wa mfanyabiashara marehemu na akaapa kwamba hatapumzika hadi haki itakapotekelezwa.

“Ningependa kutoa pole nyingi kwa familia, marafiki wa Bwana Kitonga na kwa kweli watu wa Kitui Mashariki kwa hasara hii mbaya na chungu. Nafsi yake ipumzike kwa amani ya milele,” Ngilu alisema

NTV kwa upande wao ilidai kuwa watu wawili wasiojulikana walitekwa nyara wakati wa shambulio la Jumapili huko Endau.

“Hali ya taharuki imetanda katika kaunti ya Kitui baada ya watuhumiwa wa majambazi wenyeji wa Somalia kumuua mfanyabiashara wa ndani na kuwateka watu wawili,” kituo cha KiKamba kiliripoti.

Tukio hili linakuja siku chache baada ya gavana wa Kitui kujikuta katika hali mbaya kufuatia kutokea kwa rekodi ya sauti ambamo anaonekana kuchochea wenyeji dhidi ya wachungaji wa Kisomali katika kaunti yake.

Kwenye rekodi hiyo ambayo inasemekana kurekodiwa mnamo mwaka wa 2018, anasikika akiwaambia wakazi wake kwamba kuwapa mafunzo ya kupambana na wachungaji wa Somalia. Kufikia sasa, Wabunge wanane wa Bunge kutoka Kaskazini mwa Kenya wanataka Gavana wa Kitui Charity Ngilu kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *